Maafande wa Jeshi la Kujenga Taifa ‘JKT Tanzania’ waliorejea Ligi Kuu Bara kwa msimu ujao wameanza fujo za usajili kwani tayari wana majina mawili ya wachezaji ambao wanataka kuwasajili kwa ajili ya kuwatumia msimu ujao.

Inadaiwa kuwa tayari mabosi wa JKT Tanzania ina majina ya Deusdedith Okoyo (Geita Gold) na Kassim Haruna Tiote’ (Namungo) kwa ajili ya msimu ujao. Wawili hawa wote waliwahi kufanya kazi na kocha wa sasa JKT Tanzania, Malale Hamsini walipokuwa Polisi Tanzania.

Imefahamika kuwa upande wa Okoyo tayari alishatumiwa nauli na JKT Tanzania kwa ajili ya kutua jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kumalizana.

Mtu wa karibu na bosi wa JKT Tanzania amesema Okoyo ni miongoni mwa wachezaji ambao wamependekezwa na kocha wao mkuu.

“Sio tu Okoyo ambaye amependekezwa, yupo pia Tiote na hii anawataka kwa sababu ya kutengeneza timu iliyo bora na kuleta ushindani kwenye Ligi Kuu,” kimesema chanzo hicho.

Okoyo ambaye anacheza kwenye eneo la kiungo alikuwa mchezaji anayeanza kwenye kikosi cha kwanza alipokuwa akiitumikia Geita Gold lakini tayari ameshamaliza mkataba wake. Upande wa Tiote yeye hajawa na uhakika wa namba katika kikosi cha cha kwanza cha Namungo.

Serikali yafungia Hospitali 46 kwa kutoa huduma kienyeji
Cedric Kaze aigomea Young Africans