Gwiji wa Soka nchini England na Beki wa zamani wa klabu ya Manchester United Rio Ferdinand amesema klabu hiyo ipo kwenye hatua za mwisho kununuliwa na wamiliki wa Qatar.

Ferdinand ameyazungumza hayo akisema kutoka katika vyanzo vyake vya kuaminika ununuzi wa klabu ya Man United upo karibuni na wanunuzi watakua kutoka Qatar ambao wamekua wakihusishwa kuinunua klabu hiyo wakiongozwa na Sheikh Jassim.

Beki huyo wa zamani wa klabu hiyo anasema anaomba wamiliki wa klabu hiyo familia ya Glazers wahakikishe wanakamilishe mchakato huo haraka ili klabu hiyo iweze kufanya usajili vizuri katika dirisha hili kubwa ambalo limefunguliwa jana Ijumaa (Juni 16).

Klabu ya Man United iliwekwa sokoni kuanzia mwaka jana mwishoni na wamiliki wa klabu hiyo familia ya Glazers ambapo mchakato wa kuinunua klabu umedumu kwa takribani miezi sita, huku taarifa zikieleza Glazers ndio wanakwamisha dili hilo kukamilika.

Ferdinand pamoja na magwiji wengine wa klabu hiyo wamekua wakitamani Glazers waiachie timu hiyo kwani anaona ni kama wamefeli kuiongoza klabu hiyo siku za hivi karibuni na klabu hiyo imekua ikiporomoka siku hadi siku kiwanjani.

Morrison: Young Africans ni zaidi ya Kaizer Chiefs
Fursa kimaendeleo: Mbunge ataka vikundi imara vya Bodaboda