Maadhimisho Siku ya Kimataifa ya kupiga vita dawa za kulevya ambayo kitaifa yatafanyika Juni 25 mwaka huu jijini Arusha, ambapo mgeni rasmi anatazamiwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Hayo yamebainishwa hii leo Juni 19, 2023 jijini Dar es Salaam na Kamishina Jenerali wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya, Aretas Lyimona kudai kuwa Mamlaka hiyo inawataarifu watu wote kuwa, Juni 26 Juni kila mwaka.

Amesema, lengo la siku hiyo ni kuongeza uelewa wa jamii na kuhamasisha Umma kushiriki katika mapambano dhidi ya matumizi na biashara ya dawa za kulevya huku akifafanua maadhimisho haya kwa mwaka huu kitaifa, yatafanyika kuanzia Juni 23 Juni, hadi Juni 25 2023 jijini Arusha.

Aidha ameongeza kuwa, “maadhimisho haya yataambatana na maonesho ya shughuli mbalimbali za udhibiti zinazofanywa na Mamlaka pamoja na wadau wake katika udhibiti wa dawa za kulevya na utoaji elimu na Tanzania huungana na mataifa mengine kuadhimisha Siku ya Kimataifa ya Kupiga Vita Dawa za Kulevya Duniani.”

Dkt. Tax awapa neno la shukrani Mabalozi
Bangala amtaja Ibenge Young Africans