Jeshi la Polisi nchini Uganda, linawashikilia watu 20 kwa tuhuma za kushirikiana na kundi la wanamgambo waasi linalodaiwa kufanya shambulio wiki iliyopita katika shule iliyoko jirani na mpaka wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Kwa mujibu wa Msemaji wa Polisi nchini humo, Fred Enanga amesema watuhumiwa hao 20 walikamatwa wakishukiwa kushirikiana na waasi hao wa kikundi cha Allied Democratic Forces – ADF, chenye makazi yake nchini DRC.

Sehemu ya Waombolezaji katika mazishi ya baadhi wa wanafunzi wa Sekondari ya Mpondwe. Picha ya Stuart Tibaweswa/AFP.

“Pia Mwalimu Mkuu na Mkurugenzi wa Shule ya Sekondari husika tunao, ikiwa kama sehemu ya uchunguzi wetu. Wanatakiwa watupe majibu ya baadhi ya maswali ili kupata ukweli,” aliongeza, bila kufafanua iwapo na wao wamewakamata.

Hata hivyo, Enanga alisema idadi ya watu waliouawa katika shambulio hilo lililofanyika katika shule ya Sekondari ya Lhubiriha iliyoko Mpondwe katika eneo la Magharibi mwa Uganda siku ya Ijumaa imefikia 42, wakiwemo wanafunzi 37.

Aliyekimbiwa na mke kisa hana fedha ajikuta njia panda
Dereva aliyesababisha ajali Moro akamatwa