Balozi wa Kenya Nchini Tanzania, Izack  Njenga amesema kwa kipindi kilichopita wafanyakazi wa Serikali za Kenya na Tanzania wakiwemo watekelezaji, hawakuwa na ufahamu na hawakuangalia ama kufanyia kazi suala la upitishaji wa bidhaa mpakani hasa zao la Mahindi.

Balozi Njenga ameyasema hayo wakati akizungumza na Dar24 Media hivi karibuni na kudai kuwa Kenya inakusudia kukutana na Waziri wa Kilimo wa Tanzania, Hussen Bashe, ili kuona namna ya kupata mfumo rahisi kwa wafanyabiashara kujisajili na kuweza kupata kibali (Expot Permit), kwa njia rahisi ili kuondoa ufisadi ulipo mpakani.

Amesema, “tunatumia wote mfumo mmoja wa kurahisisha usafirishaji (single custome territory) na ukiangalia mipaka yetu mingi kituo kimoja kinatumiwa na watanzania na wakenya inaitwa (one stop border point), na shughuli zote zinafanywa kwa pamoja na hii imesaidia.”

Balozi wa Kenya Nchini Tanzania, Izack  Njenga.

aidha, Balozi Njenga ameongeza kuwa “Rais Samia Suluhu Hassana amekuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha kuwa watu wanafanya kazi pamoja na maafisa wetu ambao wanatekeleza shughuli za kibiashara pale, lazima waelewe kazi yao ni kufanikisha na kurahisisha sio kuzuia.”

“Bidhaa ya mahindi ama nafaka kwa ujumla ni bidhaa ambayo inahusiana na suala zima la usalama wa Taifa maana yake ni chakula muhimu ambacho watu wengi wanakitumia na bei yake ikipanda ama kushuka au ikikosekana basi itaumiza watu wengi maana ni chakula ambacho kinapatika kwa urahisi katika nchi ama ni nafuu kwa watu wengi,” ameongeza.

Hata hivyo, Balozi Njenga amesema Serikali zote mbili (Tanzani ana Kenya) zinatoa kibali bure na kudai kwamba “tunajua hilo lakini kwasabau hazipatikani kwa uraisi huyu dalali anakwambia kwamba kibali ni shilingi laki tatu wakati msimu unaendelea na ‘demand’ inaendelea kuwa juu wanapandisha mpaka hivi majuzi ilifika laki nane.”

Rais Young Africans awatuliza mashabiki, wanachama
Asimulia mwanaye alivyosajiliwa kumuabudu shetani