Bosi wa Singida Fountain Gate (SFG), Olebile Sikwane amesema msimu ujao watahakikisha wanaendelea kusalia katika nafasi nne za juu kwenye Ligi Kuu.

Singida ina mipango ya kuwa miongoni mwa timu bora kwa lengo la kuleta ushindani ndani na nje ya nchi katika mashindano ambayo inashiriki kwa kuwa na viongozi wazuri wanaojua soka la Afrika.

Silowane ni mmoja wa viongozi waliotangazwa juma lililopita akipewa nafasi ya mtendaji mkuu wa timu.

Bosi huyo amesema watahakikisha timu hiyo inaendeleza pale ilipoishia msimu uliopita na hilo litawezekana kwa kila mmoja kuonyesha uwezo wake.

“Tunatakiwa pia kufanya vizuri katika mashindano yetu ya CAF kwenda kushindana na sio kushiriki. Nitatengeneza nguvu kubwa ya mashabiki Singida ambayo itatusaidia katika kutengeneza kipato na kukuza mtandao wa timu kwa kuwa na wadhamini,” amesema

Sikwane alisema wakiwa na wadhamini maana yake watapata na wachezaji bora na kutengeneza timu bora yenye maendeleo na wachezaji wa baadaye.

Katika yote haya inawezekana kwa kuwa na watu ambao ni bora (staff) ambao tunashirikiana,” amesema

CAG abaini dosari uendeshaji masoko ya Samaki
Simba SC kumpotezea Muethiopia