Takriban watu 41 wameuawa katika gereza la wanawake nchini Honduras kufuatia kuzuka kwa mapigano baina ya magenge hasimu, yaliyopelekea kuzuka kwa moto ndani ya jengo la wafungwa.

Naibu Waziri wa Usalama wa nchi hiyo, Julissa Villanueva ametangaza hali ya hatari na kuahidi kukabiliana na ghasia hizo na kuidhinisha Polisi, zimamoto na wanajeshi kuingilia kati huku akisema, “hasara ya maisha ya binadamu haitavumiliwa.”

Maafisa katika gereza hilo, wanasema moto huo ulisababisha vifo vingi lakini baadhi ya waathiriwa walipigwa risasi huku wengine wakiwahishwa Hospitali kwa matibabu.

Haijulikani ikiwa wote waliouawa walikuwa ni wafungwa wa jela hiyo, ambayo iko takriban kilomita 20 kutoka mji mkuu wa Honduras, Tegucigalpa, na inashikilia karibu watu 900.

Mbeya City yaahidi kubaki Ligi Kuu
Ziyech, Koulibaly kufungashiwa virago Chelsea