Aliyewahi kuwa Kocha Mkuu Simba SC Didier Gomes Da Rosa anatajwa kutuma maombi kwa Mabingwa wa Soka Tanzania Bara Young Africans, ili kuchukuwa nafasi ya Nasreddine Nabi aliyeondoka klabuni hapo, kufutia mkataba wake kufikia kikomo.

Chanzo cha habari kutoka ndani ya Young Africans kimeeleza juu ya kocha huyo wa zamani wa Simba SC kutuma CV ndani ya klabu hiyo akitaka kurejea kufundisha soka Tanzania kwa mara ya pili.

“Makocha wengi wametuma tayari CV zao wakitaka kuifundisha Young Africans, makocha wapo wengi sana tena wengine ni wakubwa mno na wengine hadi wamewahi kufundisha Simba SC lakini hilo kwao hawalijali.

“Moja kati ya hao makocha ni pamoja na Didier Gomes ambaye amewahi kuifundisha Simba SC ni moja ya makocha ambao wametuma CV zao, kwa sasa ni suala la ungozi kuona wanaamua vipi katika mchakato wa kumpata kocha mpya na tunawaachia.” Kimeeleza chanzo hicho

Oktoba 26, 2021 Klabu ya Simba SC ilitoa taarifa kuwa imeridhia ombi la Gomes kuondoka klabuni hapo baada ya tathmini na majadiliano ya kina kwa pande zote.

Kuondoka kwa Gomes kulikuja siku chache baada ya timu hiyo kuondoshwa kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Jwaneng Galaxy ya Botswana walipokubali kichapo cha mabao 3-1, katika Uwanja wa Benjamin Mkapa.

Young Africans mpaka sasa bado hawajatangaza jina la kocha mpya huku taarifa zikidai kuwa zaidi ya makocha 1000 walishatuma CV zao wakitaka kuifundisha timu hiyo.

Luis Enrique kukabidhiwa mikoba PSG
Brendan Rodgers: Nimerudi kwa heshima kubwa