Boniface Gidoen – Tanga.

Maofisa wawili wa Halmashauri ya Wilaya ya Korogwe iliyopo Mkoani Tanga, wamepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Wilaya wakishitakiwa kwa makosa matano ikiwemo kutuma nyaraka za uongo na ya uhujumu uchumi.

Maofisa hao, ni Gregory Matandiko, Afisa Ugavi Halmashauri ya Wilaya ya Korogwe, na Yasini Msangi, Afisa Mipango Halmashauri ya Wilaya ya Korogwe ambao hati yao ya mashitaka imesomwa Juni 21, 2023 mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi wa Mahakama ya Wilaya ya Korogwe, Flora Bhalijuye.

Wakiwa Mahakamani hapo, mbele ya Wakili wa Serikali wa Ofisi ya Taifa ya Mashitaka, Sarah Wangwe akishirikiana na Mwendesha Mashitaka wa TAKUKURU Doreen Kaskazi, walisomewa makosa mawili ya kutuma nyaraka ya uongo kwa lengo la kumpotosha muajiri kinyume na kifungu cha 22 cha Sheria ya kuzuia na kupambana na rushwa Sura ya 329 marejeo ya mwaka 2022.

Makosa mengine matatu, wanatuhumiwa kuhalalisha nyaraka ya uongo kinyume na kifungu cha 342 cha Sheria ya kanuni ya adhabu Sura ya 16 marejeo ya mwaka 2022, na kesi hiyo imeahirishwa hadi Julai 20, 2023 kwa ajili ya kusoma hoja za awali, huku washtakiwa wakiwa nje baada ya kukidhi vigezo vya dhamana.

Idadi waliofariki ajali Basi la New Force yaongezeka
Mtihani ni lazima kabla ya usaili