Mwenyekiti wa Mtandao wa Kijinsia – ZGC, Asha Aboud ameipongeza TAMWA-ZNZ kwa kutayarisha na kuzindua muongozo wa sera ya kijinsia na kuwataka wakuu wa vyuo vikuu nchini na dawati la kijinsia kuitumia ili kuepusha rushwa ya ngono ambayo moja ya athari zake ni kutoa wasomi wasio na sifa

Asha Aboud ametoa pongezi hizo wakati wa uzinduzi rasmi wa muongozo wa sera ya jinsia uliofanyika ofisi za TAMWA ZNZ, Tunguu Mkoa Kusini Unguja na kusema imezinduliwa ili kutekeleza mradi wa kuwawezesha wanawake kushika nafasi za uongozi (SWIL).

Awali, Mkurugenzi wa Chama cha Waandishi wa Habari Tanzania TAMWA ZNZ, Dkt. Mzuri Issa, aliwataka wadau wa masuala ya maendeleo ya jinsia kutumia muongozo wa sera ulioandaliwa kwa ajili ya vyombo vya habari ikiwemo vyuo vikuu, taasisi za serikali na binafsi kuweza ufikiaji wa usawa wa kijinsia.

Amesema, atua hiyo itasaidia kutambua kanuni zitakazoundwa na chombo cha habari, na kuipa mamlaka dawati kusikiliza na kupokea taarifa mbalimbali za unyanyasaji wa kijinsia ili kuchukua hatua kwa wahusika kama moja ya ukomeshaji wa jambo hilo.

Kwa upande wake, Katibu Mtendaji wa Tume ya Utangazaji Zanzibar, Suleiman Abdallah amesema ni muhimu kwa vyombo vya habari kufuata na kutumia muongozo huo wa sera ya jinsia ili kuweza kuweka usawa wa kijinsia katika maeneo ya kazi, na kuondosha changamoto zinazowakabili wanawake.

Lamin Jarjou kusajiliwa jumla jumla Azam FC
Rais Young Africans awatuliza mashabiki, wanachama