Aliyekuwa Kiungo Mshambuliaji wa Real Madrid, Eden Hazard, amefunguka kuwa bado ana nguvu ya kuendelea kucheza soka la ushindani.

Hazard bado haijafahamika msimu ujao atakuwa katika klabu gani baada ya kuondoka Real Madrid ambapo alikuwa na kikosi hicho tangu 2019.

Staa huyo aliyejiunga na Madrid akitokea Chelsea, ameshindwa kuonesha makali yake klabuni hapo kutokana na kutumia muda mwingi kuuguza majeraha.

Tayari nyota huyo alitangaza kustaafu kuichezea timu ya Taifa ya Ubelgiji na hivi karibuni aliagwa rasmi.

Hazard amesema: “Nawahakikishia kuwa bado nina nguvu ya kucheza soka la ushindi bila tatizo kwani mwili wangu kwa sasa uko vizuri.

“Nimepumzika kwa miaka mitatu, ndiyo maana nasema bado nina nguvu ya kupambana uwanjani na sina hofu kwa hilo.”

Waziri Mkuu akiri uwepo wa mapungufu Bandari Dsm
Mchezaji mpya kutangazwa Jumamosi