Baada ya kupewa mkono wa kwaheri ndani ya kikosi cha Mabingwa wa Soka Tanzania Bara Young Africans, Kiungo Mshambuliaji Dickson Ambundo kuna uwezekano mkubwa akarejea katika kikosi cha Dodoma Jiji FC.

Ambundo anaingia kwenye rekodi ya kuwa mzawa aliyeingia kwenye orodha ya wachezaji waliofika katika hatua ya Fainali ya Kombe la Shirikisho Barani Afrika na kugotea nafasi ya pili.

Pia akiwa Young Africans ni miongoni mwa waliotwaa mataji ya ligi mara mbili ikiwa ni msimu wake wa kwanza 2021/22 na 2022/23 baada ya kujiunga na timu hiyo akitokea Dodoma Jiji FC.

Taarifa zinaeleza kuwa Dodoma Jiji FC wapo kwenye mpango wa kufanya maboresho kwenye kikosi hicho na miongoni mwa nyota wanaotajwa ni pamoja na Ambundo.

Ikumbukwe kwamba kwa msimu wa 2022/23 Ambundo akiwa na uzi wa Young Africans alicheza mechi 13 na kukomba dakika 454 alitoa pasi moja ya bao.

Afisa Habari wa Dodoma Jiji FC, Moses Mpunga amesema kuwa mipango yao ya usajili kuelekea msimu mpya wa 2023/24 iko vizuri na wanatarajia kuwa na kikosi bora na imara.

“Kuhusu usajili wa nani atakuja ama nani ataondoka ni ripoti ya benchi la ufundi itasema hivyo ni jambo la kusubiri na kuona.”

Ikumbukwe kuwa Ambundo kabla ya kutua Young Africans alitokea Dodoma Jiji.

Julai 21 siku maalum ya Lionel Messi Marekani
Waziri Mkuu akiri uwepo wa mapungufu Bandari Dsm