Imefahamika kuwa, Klabu ya Inter Miami inatarajiwa kumtambulisha staa wake mpya, Lionel Messi, Julai 21 mwaka huu.

Messi ambaye kwa sasa yupo katika majukumu na timu ya Taifa ya Argentina, tayari anatambulika kama mcheza wa Inter Miami ya Ligi Kuu ya Marekani.

Staa huyo ametua Inter Miami baada ya kumaliza miaka yake miwili ndani ya Klabu ya Paris Saint-Germain huko Ufaransa.

Inaelezwa kuwa, siku maalum ya kumtambulisha staa huyo mbele ya mashabiki na viongozi wa klabu hiyo itakuwa Julai 21, mwaka huu huko Marekani.

Hii inakuwa ni mara ya kwanza kwa Messi kucheza soka la ushindani nje ya Ulaya.

Mshindi huyo wa Ballon d’Or mara saba, atakuwa ndani ya uzi wa Inter Miami kwa msimu wa 2023-24, huku akiacha alama kubwa katika soka la Ulaya akishinda mataji yote aliyoshindania, sambamba na Kombe la Dunia 2022 akiwa na Argentina.

Makala: Liko wapi tumbo lililozaa waasisi Afrika
Ambudo atajwa Dodoma Jiji FC