Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt Tulia Ackson ameitaka Serikali kugawa magari ya wagonjwa kwa kuangalia jiografia na idadi ya watu, ili kuweza kukidhi mahitaji ya eneo husika tofauti na utaratibu uliopo wa kuyagawa kwa kila Halmashauri.

Spika Dkt. Tulia ameyasema hayo hii leo Juni 22, 2023 wakati wa kipindi cha maswali na majibu Bungeni jijini Dodoma.

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt Tulia Ackson.

Amesema, “magari mawili kwa kila halmashauri, lakini Halmashauri nyingine ni ndogo sana. Moja kwa moja peleka kila Halmashauri sawa lakini yale yanayobaki tazameni kuna Halmashauri ni kubwa sana zipewe hata matatu.”

Mosimane ampa kazi Nabi Kaizer Chiefs
Ibrahim Ajibu atuma salamu Ligi Kuu