Watu wote watano wamefariki wakiwa ndani ya chombo cha majini kilichotoweka kikiwa karibu na mabaki ya meli ya Titanic, ambacho kilikuwa kikitafutwa tangu Juni 18, 2023 ambapo inadaiwa kilipasuka kutokana na shinikizo kubwa la maji ya bahari.

Taarifa ya Maafisa wa idara ya walinzi wa pwani ya Marekani, imeeleza kuwa tayari wamezifahamisha familia za watu waliokuwa ndani ya chombo hicho, kuhusu na mkasa huo, baada ya mabaki yaliyopatikana wakati wa utafutaji wa chombo hicho kuashiria kilipata ajali mbaya.

Taarifa hiyo iliyosainiwa na Admirali John Mauger, imezidi kueleza kuwa pia Kampuni ya OceanGate Expeditions, inayomiliki chombo hicho, iliufahamisha umma kuwa watu wote watano waliokuwa ndani, akiwemo Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Stockton Rush, wanaaminika kuaga dunia.

Katika utafutaji huo, vipande vitano tofauti viligunduliwa ambavyo viliruhusu mamlaka kuthibitisha kuwa vilitoka kwa Titan, ikiwa ni pamoja na sehemu ya nyuma ya chombo hicho, kufuatia juhudi kubwa za utafutaji wa kimataifa iliyohusisha vikosi vya Marekani, Kanada, Uingereza na Ufaransa.

Hata hivyo, shughuli za kutafuta mili ya watu hao zinaendelea na ikumbukwe kuwa OceanGate imekuwa ikirekodi hali ya kuoza kwa meli ya Titanic na mfumo wa ikolojia wa chini ya maji unaoizunguka kupitia safari za kila mwaka tangu mwaka 2021.

Wakala wa Ranga Chivaviro amaliza utata
Habari Kuu kwenye magazeti ya leo Juni 23, 2023