Mabingwa wa Soka nchini Uganda Vipers SC  wameingia makubaliano ya ushirikiano na klabu ya soka ya Wanawake ya Wakiso Hills ikiwa ni kutekeleza agizo la kikanuni la leseni za vilabu kutoka Shirikisho la Soka Barani Afrika ‘CAF’.

Kwa mujibu wa kanuni mpya za CAF, klabu yoyote itakayopata nafasi ya kushiriki mashindano ya Afrika kuanzia msimu wa 2023/24, itapaswa aidha kuwa na timu ya Wanawake au kushirikiana katika uendeshaji na taasisi nyingine yenye timu ya Wanawake.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka nchini Uganda, ni rasmi sasa Vipers SC wanafanya kazi kwa ushirikiano na Wakiso Hills kuanzia msimu ujao.

“Wakiso Hills itakuwa timu rasmi ya Wanawake ya Vipers katika shughuli zote za FUFA, CAF na FIFA.

“Vipers SC inakaribisha kwa moyo mkunjufu Klabu ya Soka ya Wanawake ya Wakiso Hills kwa Timu Moja” imeeleza taarifa hiyo kutoka Uganda

WAKISO HILLS

Wakiso Hills ilianzishwa mwaka wa 2010 kama timu ya shule ya Wasichana ilikuwa mojawapo ya taasisi za waanzilishi wa Ligi ya FUFA Women Elite mwaka wa 2015.

Wakiso Hills ilimaliza nafasi ya pili katika ligi iliyomalizika hivi punde ya Wanawake kwa kukusanya pointi 37 katika mechi 18 na hivyo kupanda moja kwa moja hadi FWSL ya msimu ujao.

Ya kuongeza nguvu za kiume yapigwa marufuku
Shubiri vita ya Ukraine Wagner ikiapa kuirudi Urusi