Dawa ya Kinywaji kitwacho Akayabangu ambayo inadaiwa kuchanganywa na Dawa mbalimbali aina ya Viagra na kutumika kwa ajili ya kuongeza nguvu za kiume, imefungiwa na Baraza la Tiba asili na Tiba mbadala.

Mwenyekiti wa Baraza hilo, Prof. Hamisi Malebo amesema hatua hiyo inafuatia uchunguzi wa baraza hilo ambao umebaini kuwepo kwa kinywaji hicho ambacho kimetengenezwa na kuanza kuuzwa bila kupewa kibali na mamlaka husika.

Amesema, hadi sasa Baraza limesajili waganga tiba asili na tiba mbadala 43,854 na vituo 1,375 hivyo kutoa onyo kwa wauzaji wa Dawa za asili wanazotembeza mitaani bila kuwa na kibali kwani ni kinyume na utaratibu.

“kufanya hivyo ni kosa kisheria hivyo kwa Mtu yoyote atakaye kamtwa hatua Kali zitachukuliwa dhidi yake na tunawatahadharishwa Wananchi kutonunua Dawa kwenye vituo visivyosajiliwa kwani wanaweza kupata madhara kutokana na Dawa hizo kuchanganywa kienyeji bila kipimo,” amesema Prof. Malebo.

Baraza la Tiba asili na tiba mbadala ni chombo cha Serikali nchini, kilichoundwa mwaka 2005 chini ya sheria ya Tiba Asili na Tiba mbadala na 23 ya mwaka 2002, kikilenga kusimamia, kudhibiti, kuratibu na kuendeleaza huduma za tiba asili na tiba mbadala.

Azam FC yamkana Bernard Morrison
Vipers SC yazifuata Singida Fountain Gate, Azam FC