Mshetani Wekundu ‘Manchester United’ wanatarajia kutuma ofa ya mwisho yenye thamani ya Pauni 55 milioni kwa ajili ya kiungo kutoka nchini England na klabu ya Chelsea Mason Mount.

Maamuzi hayo yamefikiwa baada ya ofa yao ya pili ya Pauni 45 milioni pamoja na nyongeza ya Pauni 5 milioni kukataliwa na The Blues.

Kwa mujibu wa ripoti iliyotolewa na Fabrizio Romano, Meneja wa Man Utd Erik ten Hag anadhani kiwango hicho cha pesa ni kikubwa, na endapo watashindwa kukubaliana watajiondoa kwenye mbio za kuwania saini yake.

Mount, ambaye ameichezea The Blues mechi 200, alichaguliwa kuwa Mchezaji Bora wa Mwaka wa Chelsea kuanzia msimu wa 2020-21 na 2021-22, lakini sasa imeonekana wazi hana mpango wa kukipiga Stamford Bridge msimu ujao.

Mount aliisaidia Chelsea kubeba ubingwa wa Ligi Mabingwa Ulaya mwaka wa 2021, alifunga mara mbili dhidi ya Porto na Real Madrid kwenye mechi ya robo fainali.

Kiwango cha mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24 kimetatizwa na majeraha ya mara kwa mara msimu uliopita, na akafanyiwa upasuaji wa goti.

Chelsea ilijaribu kufanya mazungumzo ya mkataba mpya na Mount, Februari mwaka huu lakini hawakufikia makubaliano kwenye mshahara.

Mchezaji huyo wa kimataifa wa England ni mmoja kati ya kiungo ambaye ataondoka kwenye dirisha hili la usajili la kiangazi na atataka akipige Man United msimu ujao.

Hofu ya Nketiah yaziita West Ham, Crystal Palace, Fulham
Simba SC kushusha nyanda la Kibrazil