Mbunge wa Jimbo la Kapseret, Oscar Sudi amesema endapo atapewa Ridhaa ya kuongoza Taifa la Kenya kwa siku tatu atakomesha maandamano ambayo yamekuwa yakiratibiwa na Kiongozi wa Upinzani, Raila Odinga.

Sudi ameyasema hayo wakati akitoa ufafanuzi juu ya suala la ulipaji kodi ambalo amelifafanua kuwa Serikali haijaongeza kama watu wanavyodai bali inahimiza ulipaji ili kuweza kufanikisha mambo mbalimbali ya kimaendeleo.

Mbunge wa Jimbo la Kapseret – Kenya, Oscar Sudi.

Amesema, “Raila Odinga na timu yako, siku nikipata hii nafasi nitawanyorosha, yaani siku moja Ruto aende safari na Viongozi wote waende safari nikabidhiwe nchi yaani nitawanyorosha, haiwezekani toka nipo mtoto ni maandamano mpaka leo hatutaki vita sisi.”

Aidha, Sudi ameongeza kuwa Wananchi wanatakiwa kuzingatia kile ambacho viongozi wa Serikali wamekuwa wakihimiza, na kuongeza kuwa yale yote yaliyoahidiwa wakati wa kampeni ni lazima yafanikishwe ili kuongeza uaminifu.

Bale amtabiria makubwa Lionell Messi
KMC FC kumrudisha nyumbani David Bryson