Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, limepitisha Bajeti Kuu ya Serikali kwa mwaka wa Fedha 2023/2024 kwa kura 354 ambayo ni sawa asilimia 95 ya wabunge waliopiga kura.

Mchanganuo wa kura za bajeti ya Serikali kwa mwaka wa 2023/2024 unaonesha kuwa jumla ya wabunge waliopaswa kupiga kura ni 393, lakini waliokuwepo ni 375 pekee.

Aidha, kwa idadi hiyo ni wazi kuwa wabunge ambao hawakuwepo ni 18 pekee, huku waliopiga kuwa wakiwa ni 374 bila kura ya Spika.

Matokeo ya kura hizo yanaonesha kura za ndiyo ni 354 na za hapana 0, huku ambazo hazikuamua chochote zikiwa 20 na kufanya bajeti hiyo kupita kwa asilimia 95.

Kakolanya: Wabongo tujifunze kwa Chama, Diarra
Bila maadili maendeleo hayana maana - Msambatavangu