Uongozi wa Simba SC umemaliza hatua ya awali ya kutangaza Wachezaji wanaoachwa kwa ajili ya msimu ujao wa mashindano, na sasa inakuja na ya awamu nyingine ambayo itakuwa ni kwa wachezaji watakaowatoa kwa mkopo kwenda klabu zingine.

Wakati awamu ya pili ikitarajiwa kuanza klabuni hapo, taarifa zinaeleza kuwa huenda Beki kutoka nchini Cameroon Che Fondoh Malone mwenye umri wa miaka 24, akatua klabuni hapo kufuatia mazungumzo kati ya Uongozi wa Simba SC na Coton Sport FC kwenda vizuri.

Taarifa hizo zinaeleza kuwa, Simba SC iliwasilisha ofa ya pili kwa ajili ya Beki huyo, baada ya ile ya awali kukataliwa, na sasa mazungumzo ya usajili wa Malone yanakwenda vizuri.

Ofa ya pili ya Simba SC inadaiwa kufikia Dola za Marekani 150,000, ambazo ni sawa na Sh. milioni 359.5 za Tanzania, ili kuvunja mkataba kuvunja mkataba wa Malone.

Tayari Uongozi wa Simba SC ulishakubaliana na mchezaji kuhusu mshahara na mambo mengine binafsi ya kimkataba.

Ukikataa 'uchawa' umekataa unafiki - Mbunge
Kocha afunguka sababu za Mbeya City kushuka