Aliyekuwa Kocha wa Mabingwa wa Soka Tanzania Bara Young Africans, Nasreddine Nabi amesema ndani ya saa 48 mustakabali wake na Kaizer Chiefs utakuwa umejulikana.

Nabi aliachana na Young Africans baada ya kumalizika kwa msimu uliopita akiwa ameipa timu hiyo ubingwa wa Ligi Kuu Bara, Kombe la Shirikisho ‘ASFC’ na Ngao ya Jamii na kuifikisha fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika.

Kaizer Chiefs imekuwa ikitajwa muda mrefu kuwa inamtaka kocha huyo, lakini jana akihojiwa na The South African alisema mazungumzo yanaendelea na ndani ya saa 48 watakuwa wameshamalizana.

“Kwa sasa ni ngumu kukupa taarifa. Kwanza tunakuheshimu wewe na chombo chako cha habari, lakini tambua kuwa tunaendelea kuzungumza na viongozi wa Chiefs kupitia wakala wangu na ndani ya saa 48 tutakuwa tumeshakamilisha na kufahamu nini kinaendelea,” amesema.

Alipoulizwa kuhusu kambi ya Kaizer Chiefs, kocha huyo mwenye uzoefu mkubwa wa soka la Afrika amesema hawezi kutoa taarifa zaidi ya hiyo iliyopo, bali usubiriwe muda sahihi.

Hatujazuia biashara mazao ya Misitu - Serikali
Ukuaji wa Teknolojia: Wanazuoni walishauri Jeshi la Polisi