Kocha wa Arsenal, Mikel Arteta, amesema roho ya klabu hiyo ilikuwa imepotea kabla ya kuchukua uongozi mwaka 2019.

Arteta alikuwa kocha msaidizi wa Pep Guardiola katika Klabu ya Manchester City kwa miaka mitatu kabla ya kujiunga na Arsenal na kuwafanya washindani wa ubingwa wa Ligi Kuu msimu uliopita.

Kocha huyo mwenye umri wa miaka 41, alisema alihisi ukosefu wa uhusiano kati ya wachezaji wa Arsenal na mashabiki wakati City ilipocheza pale Emirates na alikuwa amedhamiria kubadilisha mambo.

“Hii ilianza zaidi miaka mitatu iliyopita. Nilikuwa msaidizi wa Pep kule City, tulicheza dhidi ya Arsenal na nikaona kwamba roho ya klabu ilikuwa imepotea,” alisema Arteta akiliambia gazeti la Marca.

“Haikufurahishwa, haikuhisiwa. Nilijua kwamba kulikuwa na chaguo, muda mfupi baadaye, kuwa kwenye benchi nyingine na nilijua kuwa klabu hii ni kubwa sana kwamba ilipaswa kuunganisha timu na mashabiki.

“Imekuwa vigumu kufanya hivyo, na sasa ninajisikia furaha. Tuna utambulisho wazi, kuna muungano na tumejaa nguvu. Hilo ndilo jambo kubwa zaidi. Kuanzia juu hadi chini, wote wanasukuma upande mmoja.

Msimu uliopita, timu ya Arteta ilikaribia kushinda ligi kwa mara ya kwanza tangu mwaka 2004, lakini ikamaliza katika nafasi ya pili nyuma ya City.

Arteta alisema kuwa majeraha pamoja na sare za gharama kubwa dhidi ya Liverpool, West Ham United na Southampton zilikuwa muhimu kwa mwisho mbaya wa Arsenal kwenye kampeni.

“Hadi leo, bado inaniuma sana kutoshinda Ligi Kuu baada ya ku- kaa kwa miezi 10 kupigana na City,” aliongeza.

“Sare hizo tatu mfululizo zilituadhibu, na maafa yote yaliyotokea. Kulikuwa na majeruhi watatu au wanne kwa wachezaji muhimu na kutoka hapo, kila kitu kilikuwa kigumu.

Habari Kuu kwenye magazeti ya leo Juni 28, 2023
Hatujazuia biashara mazao ya Misitu - Serikali