Wakurugenzi wanaotumia fedha za lishe kinyume na maelekezo, watachukuliwa hatua kwa kukiuka maagiza ya kuimarisha afua za lishe kwenye Mamlaka za Serikali za Mitaa.
Hayo yamebainishwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Angellah Kairuki wakati wa kufungua kikoa kazi cha tathmini ya utekelezaji wa afua za lishe kwa maafisa lishe 110 wa halmashauri zote 184 na mikoa mikoa 26.
Amesema, Wizara yake itafanya ukaguzi wa kina na maalumu wa fedha za lishe tangu Serikali ilipotoa maelekezo ya matumizi ya fedha hizi mwaka 2016 na kuwa watakaobainisha kutumia kinyume cha malengo watachukuliwa hatua.
Aidha ameongeza kuwa, anayo taarifa na kutambua baadhi ya Wakurugenzi wa Halmashauri wanaotumia fedha hizi kutekeleza shughuli zisizo za lishe kutekeleza shughuli ambazo hazihusiani na lishe jambo ambalo linarudisha nyuma juhudi za Rais.