Serikali nchini, imeongeza vituo vyenye vyumba maalumu kwa ajili ya kutoa huduma kwa watoto wachanga wenye umri kati ya sifuri mpaka mitano wenye hali mahututi, (Neonatal Care Unit), kutoka 18 mwaka 2017 kufikia 175 mwaka 2023.

Hayo yamebainishwa na Naibu Waziri wa Afya, Dkt. Godwin Mollel hii leo Juni 28, 2023 wakati akijibu swali la Mbunge wa viti maalumu, Zaytun Seif Swai Bungeni Jijini Dodoma na kusema pia imeendelea kutoa mafunzo kwa watoa huduma kutoa huduma jumuishi kwa watoto wachanga na watoto wakubwa ili kuokoa vifo vinavyoweza kuepukika.

Amesema, “Serikali pia kupitia Wizara ya Afya imeendelea kutoa mafunzo kwa watoa huduma juu ya namna ya kutoa huduma jumuishi kwa watoto wachanga na watoto wakubwa (Intergrated Management of Childhood Illness-IMCI) ili kuokoa vifo vya watoto hao vinavyoweza kuepukika,” amesema Mollel.

Aidha ameongeza kuwa, Serikali imeendelea kuimarisha huduma za kukinga na kuzuia magonjwa yanayozuilika kwa Chanjo kama vile Surua, Nimonia, kuharisha, donda koo, kifaduro, pepo punda na polio kwa kuongeza utoaji wa chanjo za Watoto chini ya Mwaka mmoja kufikia kiwango cha zaidi ya asilimia 98 ya utoaji wa chanjo ya Penta 3.

Young Africans yakanusha kufungiwa FIFA
Simba SC yafunguka Thank You ya Sawadogo