KLabu ya Liverpool imepanga kuifumua safu yao ya kiungo kwenye dirisha hili la uhamisho wa majira ya kiangazi baada ya chama hilo la Kocha Jurgen Klopp kufanya hovyo msimu uliopita na kushindwa kufuzu kucheza Ligi ya Mabingwa Ulaya kwa msimu ujao.

James Milner, Alex Oxlade-Chamberlain na Naby Keita tayari wameshaondoka bure kabisa kwenye kikosi hicho, huku wenyewe wakimwongeza kiungo Alexis Mac Allister kutoka Brighton.

Zaidi, Liverpool inahusishwa na viungo wengine wa moto akiwamo Nicolo Barella, Ryan Gravenberch na Khephren Thuram.

Hata hivyo, Liverpool inaweza kuokoa mamilioni ya pesa kama itamtumia kiungo kinda Curtis Jones.

Kocha Klopp aliwahi kumsifia Jones kuwa ni kiungo wa kiwango cha dunia kutokana na kiwango chake alichokionyesha kwenye mechi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya FC Porto mwaka 2021.

Hata hivyo, kiwango cha mkali huyo kilidhorota msimu uliopita. Jones alikosa zaidi ya miezi miwili kutokana na kusumbuliwa na majeruhi.

Lakini, alirudi kwa nguvu mpya mwishoni mwa msimu na katika mechi 11 za mwisho za Liverpool ilizocheza kwenye Ligi Kuu England alichangia mabao manne.

Wachambuzi wa soka wanaamini kama Klopp atatoa nafasi kwa Jones basi jambo hilo litawafanya kuokoa pesa nyingi wanazotaka kutumia kwenye usajili, hasa ukizingatia msimu ujao hawapo kwenye mikikimiki- ki ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Abdihamid Moallin ahusishwa kutua Tanga
Makocha watatu wanaswa Msimbazi