Huwezi jua ni lini utajikuta katika hali ambayo itabidi utetee heshima yako hadharani, maana kuna kisa kimoja kiliwahi kutokea ambapo Wanaume wawili walinaswa kwenye kamera wakijaribu kumkaba mpita njia kwa lengo la kumfanyia uhalifu na wakashindwa kimbinu na kumpa heshima mpita njia.

Tumezungumza na Kijana mwenye mkanda mweusi wa daraja la 2 katika sanaa ya kijeshi ya Taekwondo, kuhusu jinsi mtu anapaswa kujilinda au kuchukua tahadhari wakati na katika hali kama hiyo na ametoa vidokezo vitatu vifuatavyo:

  1. UTULIVU
    Msome mpinzani wako na mazingira aliyonayo na tafuta vitu ambavyo unaweza kutumia kama silaha ikiwa mpinzani wako atakutolea silaha kama vile kisu. Pia tafuta njia ya kumkimbia hasa ikiwa huna uwezo wa kumdhibiti au kumkabili.

Kitu kingine kama unahisi vyote huwezi yaani kumkabili au huna mbio basi jaribu kuomba msamaha ikiwa ulifanya kitu kibaya kwake, ili kushusha hasira zake au kumuepuka asikudhuru.

  1. PIGANA UKIWA MBALI.
    Watu wengi wanaona vigumu kuondoka katika hali kama hiyo na kuchanganya hatua zao na uoga. Tembea kinyumenyume huku ukimkazia macho mtu huyo, ili kuepuka kushambuliwa kwa nyuma.

Kukwepa ugomvi ni kitendo cha mtu jasiri aliyefunzwa vyema. Kutembea kunaweza kumwokoa mwanamume au mwanamke kutokana na madhila ya shambulio na uwezekano wa kufungwa jela iwapo utafanikiwa kumpiga vibaya au kumdhuru.

  1. JIFUNZE KUJITETEA
    Iwapo mshambuliaji wako atakufuata au kukushikilia sana hata baada ya kujaribu kuondoka au kumkwepa, basi una haki ya kujilinda.

Lakini kabla ya kutumia ulinzi binafsi, mpe onyo la mdomo kwa sauti kubwa uwezavyo, ili kila mtu aliye karibu asikie. Watu wa pembeni wanaweza kukuokoa na hatari au kifungo ikiwa utampiga mshambuliaji wako vibaya na ukamuumiza.

Watoto uzito pungufu: Vituo kufikia 275 Juni 2024
Singida Fountain Gate yaibomoa KMC FC