Klabu ya Manchester United imerudi tena kwenye mchakato wa kuiwania huduma ya kiungo wa Mabingwa wa Soka nchini Hispania FC Barcelona na Uholanzi, Frenkie de Jong mwenye umri wa miaka 26, ambaye kwa wakati huu itakuwa kuna ugumu zaidi kumpata kwani Bayern Munich nayo imeonyesha nia ya kutaka kumsajili.

Kocha wa Man United, Erik Ten Hag amewaambia mabosi wa timu hiyo moja ya maeneo anayotaka sana kuboresha ni hili kwani lina upungufu pia.

Man United inadaiwa kuwa kwenye mchakato wa kutaka kumuuza Donny van de Beek na mbadala wake ndio anaonekana kuwa ni de Jong.

Kumekuwa na mawasiliano mazuri baina ya kocha wa Man United na De Jong hali inayozidi kuchochea asilimia za dili hili kukamilika ingawa uwepo wa Munich huenda ukabadilisha uamuzi wa staa huyu.

De Jong ambaye mkataba wake wa sasa unamalizika mwaka 2025. Huen- da akauzwa kwa zaidi ya Pauni 70 milioni.

Kwa sasa Man United inataka kuachana na mastaa wake wengi ili kuingiza sura mpya wa ajili ya kukifanya kikosi hicho kuwa hatari kikijiandaa na msimu mpya wa Ligi Kuu England na Ligi ya Mabingwa Ulaya na msimu uliopita ilimaliza nafasi ya tatu kwenye msimamo wa EPL.

Singida Fountain Gate yajipanga 2023/24
Fidia ya ardhi: Majaliwa aziagiza Halmashauri