Kutokuwa na uhakika kwa Kocha Erik ten Hag kuhusu David de Gea kumechangia mabadiliko ya Manchester United juu ya mkataba mpya kwa Mlinda Lango huyo kutoka Hispania.

Mail Sport ilifichua mapema mwezi huu kwamba mfumo wa mkataba mpya unaolenga kupunguza mshahara wa De Gea wa Pauni 375,000 kwa juma ulikubaliwa kati ya mchezaji huyo na klabu, lakini kutoridhishwa kwa Ten Hag juu ya kiwango cha namba moja wake huo kumeweka dili hilo hatarini.

Ripoti ziliibuka juzi Jumanne zikidai kuwa De Gea alitia saini mkataba huo mpya kabla ya United kuunga mkono na kisha kuwasilisha ofa ndogo zaidi.

Mustakabali wa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 32 pale Old Trafford sasa unaonekana kutokuwa na uhakika zaidi kuliko hapo awali ikiwa imesalia siku moja tu tu kabla ya kuwa mchezaji huru. Mkataba wake unamalizika Juni 30.

United bado wanaweza kumsajili tena De Gea baada ya tarehe hiyo, lakini inaonekana haiwezekani katika mazingira ya sasa. Huenda matokeo ni kwamba De Gea ataondoka baada ya miaka 12 ya kukaa United na kutafuta klabu mpya huku kukiwa na ofa nono kutoka kwa Saudi Arabia.

United wamefanya mazungumzo ya kiuchunguzi kuhusu mpango wa kumnunua Andre Onana wa Inter Milan kama mbadala wake, ingawa mazungumzo ya dau la pauni milioni 50 bado hayajafikiwa.

Maofisa wa klabu walikutana na wakala wa Onana, Albert Botines, wiki iliyopita kwa majadiliano juu ya uwezekano wa kumsajili.

Wachezaji kama vile mlinda mlango wa Porto Diogo Costa, David Raya wa Brentford na chipukizi wa Anderlecht Bart Verbruggen pia wametathminiwa na United.

Usajili JKT Tanzania waanza na Wawa
Walemavu changamkieni fursa za Elimu, mikopo - Ndalichako