Walinzi wa Pwani ya Marekani limesema Wataalam wa kikosi cha ulinzi wa Pwani wamegundua mabaki ya watu wanaodhaniwa kutoka kwa Nyambizi ndogo ya Titan na kuua watu watano, ambayo ilipata ajali eneo ilipozama Meli ya Titanic.
Taaifa ya Jeshi hilo imeeleza kuwa, “Wataalamu wa matibabu wa Merika watafanya uchambuzi rasmi wa mabaki ya watu wanaodhaniwa kufariki katika ajali ya Nyambizi ya Tita ambayo yamepatikana na yatafanyiwa utafiti kwa uangalifu.”
Ajali hiyo iliwahusisha Mwanariadha Mwingereza Hamish Harding, mtaalam wa manowari wa Ufaransa Paul-Henri Nargeolet, tajiri wa Pakistani-Muingereza Shahzada Dawood na mwanawe Suleman, na Stockton Rush, Mkurugenzi Mtendaji wa OceanGate Expeditions ambao ndi wamiliki wa chombo hicho.
Inaarifiwa kuwa, chombo hicho kilipata hitilafu bada ya kupigwa na mawimbi makubwa yaliyo katika kina kirefu cha Bahari, wakati wakielekea kutalii katika Meili yo ya Titanic iliyozama mwaka 1912 ikiwa ni zaidi ya miaka 100 sasa.