Uongozi wa Simba SC umetangaza kuwa beki wao kutoka nchini Kenya, Joash Onyango Achieng, bado mali halali ya klabu hiyo, licha ya mkataba wake kubaki mwaka mmoja, huku mara kadhaa ikiripotiwa kwamba ameandika barua ya kusitisha mkataba wake huo.

Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Simba, Ahmed Ally, amesema Onyango bado ataendelea kubaki Simba kwa msimu ujao.

Ameongeza kuwa bado beki huyo anahitajika katika timu hiyo, kutokana na ubora alionao wakati wakijiandaa na michuano ya kimataifa msimu ujao 2023/24.

“Hicho kinachoendelea na uvumi tu, hakuna barua yoyote tuliyoipokea kutoka kwa Onyango ya kuomba kuondoka.

“Watu wafahamu kuwa Onyango ni mchezaji halali wa Simba SC ambaye mkataba wake unatarajiwa kumalizika msimu ujao,’ amesema Ahmed Ally.

Dodoma Jiji kumng'oa nyota wa Coastal Union
Inonga: 2022/23 ulikuwa msimu mgumu sana