Kiungo ambaye alikuwa haguswi kwa maana ya kutowekwa sokoni ndani ya kwa Real Madrid, Federico Valverde, imeelezwa kwa sasa klabu ipo tayari kupokea Euro 90m ili aende Liverpool.

Ripoti kutoka Hispania zimeeleza kuwa, Real Madrid ipo tayari kupokea kiasi hicho cha fedha kutoka kwa Liverpool kama kweli wanataka saini ya Valverde.

Valverde ni kati ya viungo bora ndani ya Madrid, huku akiwa miongoni mwa wachezaji wasioguswa sambamba na Vinicius Junior, Rodrygo Goes na Eduardo Camavinga.

Baada ya Liverpool kupiga hodi kumuhitaji nyota huyo, wameambiwa watoe kiasi cha Euro 90m ili kumpata. Real Madrid ambayo imetoka kumuuza Karima Benzema huku ikimsajili, Jude Bellingham, inatajwa kwamba timu hiyo ipo katika kujiimarisha kuelekea msimu ujao.

Vifo mfululizo familia moja vyaibua siri ya kutisha
Jurrien Timber awekewa mkakati Arsenal