Kiungo Mshambuliaji kutoka nchini Ghana Collins Opare anayekipiga ndani ya Dodoma Jiji, ameingia kwenye rada za mabosi wa Simba SC ambao wanahitaji saini yake.

Opare ni miongoni mwa mawinga wenye ushkaji na nyavu katika Ligi Kuu Tanzania Bara, aliwahi kuwafunga Young Africans walipokutana msimu wa 2022/23, huku akifunga mabao kumi kwa msimu huo.

Mtu wa karibu wa Opare, amesema kuwa, kuna ofa zaidi ya tatu zipo mezani kwake ikiwemo ya Simba SC.

“Opare ana ofa zaidi ya tatu kwa timu ambazo zinashiriki Ligi Kuu Bara, miongoni mwa hizo ni Simba SC ambayo ilikuwa inamuulizia tangu msimu uliopita.

“Kikubwa ambacho kwa sasa kinaangaliwa ni suala la maslahi na namna gani wanaweza kufikia makubaliano na mchezaji mwenyewe kwani kazi yake ni mpira,” amesema mtu huyo.

Afisa Habari wa Dodoma Jiji, Moses Mpunga, amesema kuwa: “Ni kweli wachezaji wetu walipambana kwenye ligi na kazi yao imeonakana, kuna ofa ambazo zimekuja kwa wachezaji ikiwa ni pamoja na ya Opare, hivyo ni suala la kusubiri itakavyokuwa.”

Usajili 2023/34: Mohamed Dewji aipa jeuri Simba
Vifo mfululizo familia moja vyaibua siri ya kutisha