Parachichi ni zao linalolimwa kwa wingi katika mikoa ya Kilimanjaro, Mbeya, Njombe, Songwe, Iringa, Kigoma, Tanga, Kagera na Morogoro, na kufanya Tanzania kuwa nchi ya tatu Barani Afrika kwa kuzalisha kwa wingi zao hilo, baada ya Kenya na Afrika Kusini.

Dar24 ilifanya mahojiano maalum na Balozi wa Tanzania nchini China, Mbelwa Kairuki ambaye alisema mara baada ya Rais Samia kukutana na Rais wa China, XiJinping Novemba 2022, walikubaliana kufungua soko la parachichi kwa ajili ya Watanzania.

Alisema, “mbali na Parachichi pia baadhi ya mazao yanayohitajika kwa wingi nchini China na yanazalishwa kwa wingi nchini Tanzania, ni pamoja na Maharage ya soya (soyabeans), na Wachina walikuwa wanapata soya kutoka Marekani na Brazil, sasa wanahitaji vyanzo vipya.”

Kwa mujibu wa Tanzania Horticultural Association, mwaka huu Tanzania inatarajia kupeleka nje ya nchi
tani15,000 za Parachichi zenye thamani ya Dola 45 milioni, likiwa ni ongezeko la tani 11,237 za mwaka 202.

JKT Tanzania yamnasa Hassan Nassor
Szoboszlai azingonganisha Liverpool, The Magpies