Mahakama kuu nchini Kenya, imetoa amri ya kusitisha utekelezaji wa sheria mpya ya Fedha ya mwaka 2023 ambayo ilisainiwa hivi karibuni na Rais wa nchi hiyo William Ruto.

Maamuzi hayo, yaliyotolewa na Jaji Muguru Thande wa Kitengo cha Katiba na Haki za Binadamu Milimani, na kumzuia Waziri wa Fedha, Njuguna Ndung’u, Mwanasheria Mkuu, Justin Muturi na Mamlaka ya Mapato Kenya – KRA. kuanza ukusanyaji wa tozo.

Aidha, Mahakama hiyo imetaka kuimarishwa na utekelezaji wa kuoboresha zaidi sheria hiyo ambayo ilitarajiwa kuanza kutumika rasmi hii leo Julai 1, 2023, na sasa itasubiriwa usikilizaji wa kesi iliyowasilishwa na Seneta wa Busia, Okiya Omtatah.

Amri hizo zilitolewa baada ya Omtatah na wanaharakati wengine wanne kuwasilisha maombi ya uharaka wakiomba kusimamishwa kwa utekelezaji wa Sheria mpya ya Fedha 2023 ambayo ilitiwa saini na Rais Ruto siku ya Jumatatu na kuelezea kuwa ilikuwa kinyume cha katiba.

Wanaharakati hao walimjulisha jaji kwamba sheria iliyopitshwa na utawala wa Kenya Kwanza inapelekea kuwalazimisha wakenya kulipa kodi bila ya mpangilio wala uhalali, na wanadai kodi zilizowekwa katika Sheria ya Fedha 2023 ni batili na zinakiuka kipengele cha 23 cha katiba.

Jiandaeni kujikinga na maafa -Dkt. Yonazi
Serikali yakanusha tangazo uwezeshaji Vijana