Matajiri wa jiji la Dar es salaam Azam FC, wamendelea kazi ya kuboresha mikataba ya wachezaji wao na sasa ni zamu ya, Lusajo Mwaikenda.

Mwaikenda ni chaguo la kwanza ndani ya Azam FC kwa msimu wa 2022/23 akiwa ni miongoni mwa nyota waliocheza Nusu Fainali Kombe la Shirikisho ‘ASFC’ dhidi ya Simba SC.

Kwenye ushindi wa mabao 2-1 waliopata Azam yeye alimtungua kipa namba tatu wa Simba, Ally Salim, bao moja lililofungua ukurasa kwenye ushindi na kutinga hatua ya fainali.

 Timu hiyo iliyogotea hatua ya fainali wakiwa ni washindi wa pili kwa sasa wanapambana kuboresha mikataba ya wachezaji wao pamoja na kutambulisha wapya.

Mwaikenda kaongeza dili la miaka miwili hivyo yupo ndani ya Azam FC mpaka 2025 akiungana na wenzake, Abdalah Kheri ‘Sebo’, Malickou Ndoye, James Akamiko, Sospeter Bajana ambao wameongezewa mikataba ndani ya timu hiyo.

Luis Enrique kutambulishwa Paris Saint-Germain
Ajali: Roli laparamia magari, 49 wafariki