Tume ya Taifa ya Uchaguzi imetangaza tarehe 13 Julai, 2023 kuwa siku ya uchaguzi mdogo wa madiwani katika kata 14 za Tanzania Bara ambapo uteuzi wa wagombea kwa ajili ya uchaguzi huo umefanyika jana tarehe 30 Juni, 2023.

Jumla ya Wagombea 77 kutoka vyama 14 vyenye usajili wa kudumu, wameteuliwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi kuwania nafasi wazi za udiwani katika Kata 14 za Tanzania Bara ambazo zinataraji kufanya uchaguzi mdogo Julai 13,2023.

Kati ya wagombea hao 90 waliochukua fomu, wanaume walikuwa 74 na wanawake walikuwa 16 lakini hadi dirisha la uteuzi linafungwa saa 10 kamili jioni jana ni jumla ya wagombea 77 waliteuliwa kati ya hao wanaume ni 63 na  wanawake ni 14. Aidha, jumla ya wagombea 13 hawakurejesha fomu za uteuzi.

Aidha, Katika kata 13 wameteuliwa wagombea zaidi ya mmoja, huku Kata moja ya Mnavira iliyopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Masasi mgombea mmoja tu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) ameteuliwa kutokana na wagombea wa vyama vingine kutorejesha fomu za uteuzi.

Wagombea walioteuliwa wanatoka katika vyama vya siasa 17 ambavyo ni AAFP, ACT – WAZALENDO, ADA – TADEA, ADC, CCK, CCM, CUF, DEMOKRASIA MAKINI, DP, NCCR – MAGEUZI, NLD, NRA, SAU, TLP, UDP, UMD na UPDP.

Awali Fomu za uteuzi wa wagombea hao zilianza kutolewa kuanzia tarehe 24 Juni, 2023 hadi tarehe 30 Juni, 2023 na jumla ya wagombea 90 walichukua fomu za uteuzi.

Kocha Gamondi kuamua kambi Young Africans
Jurrien Timber mambo safi Arsenal