Jamii nchini, imetakiwa kuacha matumizi ya dawa bila kupata majibu ya vipimo husika, ili kubaini aina ya ugonjwa pindi wanapokutana na changamoto za kiafya na ushauri wa tiba, kwani kitendo hicho kinahatarisha afya.

Wito huo umetolewa na Mganga mfawidhi wa kituo cha huduma za afya Susannah Wesley, Dkt. Bahati Faustine wakati wa uzinduzi wa Jengo la huduma ya Mama na Mtoto uliofanyika eneo la Kihonda mjini Morogoro.

Amesema, watu wengi wamekuwa wakijenga mazoeza ya kutumia dawa pila kupima jambo ambalo linahatarisha afya zao kwani hupata usugu wa dawa mwilini.

Awali, akizindua jengo hilo Afisa Tawala Wilaya ya Morogoro, Hilali Sagara amepongea hatua ya ujenzi wa kituo hicho ambacho kinaisaidia Serikali kutoa huduma za kiafya kwa wananchi na kumtaka mganga Mkuu Mkoani humo kutoa ushirikiano, ili waweze kutoa huduma kwa wananchi wengi zaidi.

Akizungumza kwa niaba ya mganga mkuu wa Halashauri ya Manispaa ya Morogoro, Mratibu wa huduma za afya Manispaa, Dkt. Felista stanslaus amesema wapo tayari kuunga mkono jitihada hizo kwa kutoa baadhi ya vifaa vinavyohitajika.

Jiheshimu: Mitandao si Mahakama, Ustawi wa jamii
Singida Fountain Gate yaanza kutamba