Uongozi wa Simba SC umeweka wazi kuwa kwa sasa unasaka kiungo mwenye sifa zaidi ya nne atakayeungana na timu hiyo kwa ajili ya maboresho ya msimu wa 2023/24.

Mastaa wa timu hiyo ni mashuhuda ubingwa ukienda kwa watani zao wa jadi Young Africans waliokamilisha msimu na alama 78 huku wao wakigotea kwenye alama 73.

Kinara wa pasi za mwisho ndani ya ligi ni Clatous Chama ambaye alitoa pasi 14 na alifunga mabao manne hivyo alihusika kwenye mabao 18 kati ya 75 yaliyofungwa na timu hiyo.

Kocha Mkuu wa Simba, Roberto Oliveira ‘Robertinho’ amesema anahitaji kiungo mwenye sifa zaidi ya nne atakayeongeza nguvu katika kikosi hicho.

“Unaona kuwa na kiungo kama Chama, (Clatous) hivyo ni faida mara mbili kwa kuwa anaweza kufunga, kutoa pasi na kuongeza kasi kwenye eneo la ushambuliaji na muda mwingine amekuwa akifanya kazi ya kulinda.

“Hiyo ni muhimu kwa wachezaji watakuwa ndani ya timu ni muhimu kuwa na sifa zaidi ya moja na hiyo itaongeza uimara wa kikosi na tutakuwa bora kwenye mechi za ushindani kitaifa na kimataifa hao ndio ambao tunawahitaji,” amesema kocha huyo ambaye kwa sasa yupo kwao Brazil kwa mapumziko

Matumizi ya Teknolojia: JKT liwekeze kwa Vijana - Dkt. Mpango
Abdihamid Moallin anukia Coastal Union