Wanawake hupitia msongo wa mawazo baada ya kujifungua, wengi wao wakijikuta katika hali ngumu zaidi kwa kukosa msaada wa mapema, huku watetezi wao hasa wa Afya ya akili wakisema waathiriwa wanahitaji kuzungumzia matatizo yao mapema.

Tatizo hili la huwakumba wanawake wengi hasa vijana, lakini mara nyingi huona aibu kulizungumzia wakisema sio rahisi ikiwa ndio mara ya kwanza kwa mama kujifungua na mbaya zaidi ikiwa hana wa kumuelekeza kuhusu namna ya kuikabili hali hiyo.

Jesca Mtei ni mama wa nyumbani yeye anasema, “nilinusurika na hali hiyo baada ya kukutana na rafiki yangu Thekla, alinijenga kisaikolojia na nilikaa sawa bila yeye nisingeweza kuwasaidia wengine niliweza kuwashauri wengine na nilifanikiwa, tusikae na vitu vinavyotuumiza tukiongea tunapona.”

Msongo wa mawazo baada ya Kujifungua, huathiri zaidi ya asilimia 10 ya wanawake duniani kote ingawa changamoto hii ya afya ya wanawake bado haijatambuliwa maeneo mengine Afrika na tayari Serikali imeweka mifumo ambayo inaruhusu wanawake kutafuta msaada.

Kwa upande wake Melina Alex anasema, “si magonjwa yote yanatibika kwa dawa mengine hutibika kwa maongezi tu na ukiachilia moyo wako usizongwe na mambo mengi hiyo ni afya njema mimi sijawahi kukubwa na tatizo hilo ila nimeshuhudia, nawashauri watu kuzingatia ushauri.”

Hata hivyo, Wanawake wanashauriwa kujuliana hali kabla ya kujifungua na baada kitu ambacho kitasaidia kujieleza yanayo wasibu na hatua stahiki kuchukuliwa ili kuhakikisha mambo yanakuwa sawa na kuwaepusha wengi wao kuingia katika hatari hiyo.

Nicolas Pepe afunguka maisha ya Arsenal
Ibrahim Ajibu: Wachezaji wengi waoga Ligi Kuu