Uongozi wa Azam FC umekanusha uvumi wa kuwa na mpango wa kumsajili Beki wa Kushoto wa Mabingwa wa Soka Tanzania Bara Young Africans Joyce Lomalisa Mutambala, huku ukidai unaheshimu mkataba wake.

Kwa majuma matatu sasa, tetesi za Beki huyo kutoa Azam FC zilishika kasi katika mitandao ya kijamii, huku ikidaiwa anakweda kuziba nafasi ya Mzimbabwe Bruce Kangwa, aliyepewa mkono wa kwaheri kuelekea msimu wa 2023/24.

Afisa Habari wa Azam FC, Hasheem Ibwe, amesema wanatambua ubora wa beki huyo na wanauheshimu mkataba wake na klabu yake ya sasa, na hawawezi kufanya uhuni wa kumshawishi ili ajiunge nao huko Azam Complex Chamazi.

Amesema hawana mipango ya kumsajili nyota huyo kwa sababu tayari ameshapatikana beki ambaye anakuja kurithi mikoba ya Kangwa na muda wowote watamtambulisha.

“Hakuna ukweli wa Lomalisa kwa sababu mazungumzo yameshaisha na beki kutoka Timu ya Taifa ya Cameroon ambaye alicheza CHAN, safari hii tunasajili wachezaji wanaokuja kuhakikisha tunafikia malengo yetu.

“Wakati wowote tutamtambulisha beki huyo ambaye atakuwa ni usajili wetu wa tatu wa nyota wapya baada ya hapo tutashusha kifaa kingine cha kigeni na tutafunga usajili wetu,” amesema Ibwe

Amesema wanategemea kusajili wachezaji wawili wa kigeni na wamejipanga vizuri kufanya usajili mzuri na wenye malengo kuhakikisha wanakuwa tishio kwa kutwaa mataji msimu ujao.

“Tumejipanga vizuri kwa msimu ujao na ninaimani tutafikia malengo kwa kuwa tumetimiza matakwa ya benchi letu la ufundilinaloongozwa na kocha Youssouph Dabo,” amesema Ibwe

Kocha Gamondi aanza kazi Young Africans
Thank You hazijaisha Young Africans, kukipiga Malawi