Mshambuliaji kutoka England na Klabu ya Man Utd Mason Will John Greenwood amepewa ofa ya kurejea dimbani na kocha wake wa zamani Jose Mourinho anayeinoa AS Roma, kwa mujibu wa ripoti.

Mourinho anataka mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 21 akakipige AS Roma kwa mkopo, baada ya kukaa nje kwa muda mrefu kutokana na kesi iliyokuwa ikimkabali.

Greenwood alikuwa anakabiliwa na kesi ya kutishia kuua na unyanyasi wa kijinsia, hata hivyo kesi hiyo imefutwa na mahakama, lakini bado uongozi wa Man United hawajafanya uwamuzi kuhusu hatima yake.

Kwa sasa Greenwood amepigwa ‘STOP’ na Man United huku Uchunguzi ukiendelea kuhusu tuhuma hizo licha ya mahakama kufuta kesi hiyo.

Kwa sasa Greenwood amepania kurejea dimbani aendelee na maisha yake ya soka, na kwa mujibu wa ripoti Mourinho ameonyesha nia ya kumchukua japo kwa mkopo.

Majuma kadhaa yaliyopita Greenwood alianza mazoezi binafsi ya kujiweka fiti akiwa na mwalimu wake, chanzo cha habari kimeripoti Mourinho aliwasiliana na baba mzazi wa Mshambuliaji huyo.

“Mourinho aliongea na baba yake mzazi, amemueleza njia pekee itakayomsaidia kutokana na majanga yake, kocha huyo akamwambia njia pekee Greenwood aanze kucheza soka anatamani acheze soka lakini anasubiri uongozi wa Man United utamwambia nini, timu nyingine zinazomuhitaji ni Juventus, AC Milan na Inter Milan.”

Mourinho na Greenwood wana uhusiano mzuri baada ya kumpa nafasi nyingi za kucheza wakati alipokuwa akiinoa Man United kabla ya kufukuzwa kazi.

Ikumbukwe mwaka 2018, Mourinho alimchagua Greenwood mwenye umri wa miaka 16 kipindi hicho, ashiriki maandalizi ya msimu mpya (Pre Season) yaliofanyika Marekani.

Kidunda: Ninataka kumaliza ngebe za Eric Mukadi
LATRA yaishusha ratiba ya mabasi New Force