Klabu ya Manchester United inajaribu kulipita dau la Arsenal la pauni milioni 85 kumnunua mshambuliaji wa Real Madrid, Aurelien Tchouameni.

Lakini Kocha wa Arsenal, Mikel Arteta, amemwongeza Tchouameni kwenye orodha yake fupi ya wachezaji anaowawania.

Kiungo huyo alipata shida kuwa kwenye kikosi cha kwanza katika Klabu ya Real Madrid msimu uliopita na inaaminika kuwa anaweza kupatikana kwa bei ndogo.

Kwa mujibu wa Nacional, United imeingia kwenye vita ya kutaka kumsajili mchezaji huyo wa Kimataifa wa Ufaransa, kwani pia anawaniwa na klabu kadhaa za Barani Ulaya.

Ripoti hiyo hiyo inadai kuwa bosi wa ‘Mashetani Wekundu’ hao, Erik ten Hag anaishinikiza klabu hiyo kumsajili mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 23.

Majaliwa ataka uzingatiaji maadili Viongozi wa umma
Diaspora waombwa kuchangamkia fursa za uwekezaji NSSF