Baada ya kutemwa na Mabingwa wa Soka Tanzania Bara Young Africans Wachezaji David Bryson na Dickson Ambundo wanatajwa kumalizana na Uongozi wa Singida Fountain Gate.

Ambundo alitangazwa kuachana na Young Africans juma lililopita baada ya kumaliza mkataba na timu hiyo, Upande wa Bryson yeye hadi jana Jumatatu (julai 03) bado alikuwa hajatangazwa lakini, wakati wowote Thank You yake itaanikwa hadharani.

Dili la Ambundo limekamilika na mchezaji huyo amepotezea ofa nyingi ikiwemo ya Dodoma Jiji FC na kwa sasa yupo zake Mkoani Mwanza akisubiri tu kuitwa kwa ajili ya maandalizi ya msimu mpya.

Imefahamika kuwa wachezaji hao tayari wameshasajiliwa na wapo kwenye kundi la timu hiyo mtandao wa Whatsapp kwa ajili ya kupata taarifa zote za timu hiyo kwa ajili ya msimu ujao.

Chanzo kutoka ndani ya Young Africans kimelidokeza kuwa wawili hao wapo tayari kwenye usajili wa Singida.

“Mbona tayari hao wameshaenda Singida, upande wa Bryson yeye kahusika kwenye dili la Kibabage kuja hapa Yanga kwani kuna namna ambayo imefanyika pamoja na kwamba mkataba wake umeisha,” kimesema chanzo hicho.

Upande wa viongozi wa Singida Fountain Gate, Makamu wa Rais, John Kadutu amesema kwa kifupi: “Usajili wetu tutaanza kuutangaza hivi karibuni.”

Singida inatajwa kukamilisha usajili wa kipa Beno Kakolanya (Simba SC) na Nicolaus Wadada (Ihefu FC).

Mauzo Biblia kongwe Duniani yavunja rekodi
Ajira Wahudumu wa Afya zasitishwa