Dodoma Jiji FC inawania saini ya mshambuliaji wa Coastal Union, Hamad Majimengi kwa ajili ya kuitumikia msimu ujao wa Ligi Kuu Bara.

Inaelezwa kuwa Kocha Melis Medo wa Dodoma Jiji anahitaji huduma ya mchezaji huyo kwani ana uwezo wa kucheza nafasi ya winga na mshabuliaji ili ashirikiane na wachezaji wenzake waliowahi kucheza naye Coastal Union kina Raizin Hatidh na Amani Kyata.

Katika msimu uliopita timu hiyo ilimkosa kidogo mchezaji huyo wakati akiitumikia Ruvu Shooting na ilifanikiwa kunasa saini ya Issa Abushehe pekee ambaye kwa sasa anacheza soka la kulipwa Uarabuni.

Nyota huyu alikuwa moto kwelikweli katika kikosi cha Coastal Union na aliiwezesha kukamatia nafasi ya 12 katika msimamo wa Ligi Kuu Bara licha ya kwamba kuna nyakati hakucheza kwa ama majeraha au kuwapisha wenzake kuanza kikosini na yeye kuanzia benchi.

Kwa sasa kikosi cha Dodoma Jiji kinaendelea kusukwa kwa kusajili wachezaji wapya na kuachana na ambao hawana msaada.

Jurrien Timber atahadharishwa safari ya Arsenal
Josko Gvardiol kuweka rekodi duniani