Kiungo mpya wa Liverpool, Dominik Szoboszlai aliyesajiliwa kwa Pauni 60 milioni akitokea RB Leipzig, amefichua Kocha Jurgen Klopp alitumia muda mrefu kumshawishi ajiunge na Majogoo hao dirisha hili la usajili.

Szoboszlai ni mchezaji wa pili kutua Anfield na amesaini mkataba wa miaka mitano hadi mwaka 2028 na atavaa jezi namba nane ambayo haikuwa na mtu tangu aiache lejendari wa timu hiyo, Steven Gerrard.

Szoboszlai amesema Klopp alikuwa akimpigia simu sana siku chache baada ya msimu kumalizika na kumwambia kwa nini anatakia akubali kutua Liverpool.

“Siwezi kusema tulichoongea kwenye mazungumzo hayo, lakini nilishawishika sana baada ya mazungumzo hayo.

Kwangu nilifahamu kwa nini amekuwa mmoja kati ya makocha bora Duniani, tulizungumza kana kwamba tulikuwa tunajuana kwa miaka 1000 iliyopita. Natamani sana kuanza kufanya naye kazi rasmi.”

Klopp ni mmoja wa makocha wenye ushawishi mzuri kwenye mazungumzo na hata mbinu zao hali inayosababisha wachezaji wake wawe tayari kupambana kwa ajili ya timu kupata matokeo”

Szoboszlai pia alikuwa anatakiwa na timu mbalimbali Ulaya baada ya Ligi Kuu Ujerumai kumalizika.

Fundi huyu ambaye kwenye mahojiano yake aliweka wazi kuichezea Liverpool ni moja ya ndoto zake, msimu uliopita alicheza mechi 46 za michuano yote na kutoa asisti 13.

Ndugu wadai Marehemu alikataa ushauri
Tengeru, Polisi kuja na mbinu kukabiliana na ukatili