Kiungo Jude Bellingham amefichua kuwa David Beckham alimtumia ujumbe wa kumtakia kila la kheri baada ya kujiunga na Real Madrid.

Kiungo huyo mwenye umri wa miaka 20, amekuwa mchezaji wa saba wa England kujiunga na klabu hiyo ya Bernabeu baada ya uhamisho wake wa Euro milioni 103 Kutoka Borussia Dortmund mwezi uliopita, akifuata nyayo za Beckham, Gareth Bale na Michael Owen.

Beckham labda ndiye aliyekuwa hadhi ya juu zaidi kuhamia mji huo mkuu wa Hispania mwaka 2003 kutoka Manchester United, ambao ulizidisha hadhi yake ya kimataifa, na nahodha huyo wa zamani wa England aliwasiliana na Bellingham kumtakia heri.

Na nyota huyo mpya wa Bernabeu alisema huenda akapata ujuzi wa Beckham na wachezaji wengine wa zamani wa kucheza Madrid.

“David Beckham alinitumia ujumbe mfupi wa kunitakia kila la kheri,” alisema Bellingham akiliambia Shirika la Habari la PA.

“Ni moja ya hatua ambazo kila mtu ana maoni yake kutoka nje kwa hiyo unasikia mambo mengi na ushauri, mimi ni mzuri katika kuchuja mazuri kutoka ubaya, hadi sasa imekuwa chanya kutoka kwa wachezaji wa zamani.

“Nitajaribu kuchukua hiyo kwenye bodi na wakati fulani labda nitawasiliana nao na kuona jinsi walivyozoea maisha ya Hispania.”

Moja ya mambo ambayo Bellingham atakuwa akifanya ili kuzoea mtindo wake mpya wa maisha nchini Hispania na kujifunza lugha hiyo.

Kiungo huyo ameanza kutumia programu ya kujifunzia, akilenga kuendeleza misamiati mingi ili apate nafasi ya kwasiliana bila tabu.

“Nimeiweka yote kwenye simu yangu, nina mfululízo mzuri unaoendelea dakika hii,” aliongeza.

“Ni siku tisa tangu nianze kuichukulia lugha hii kwa uzito.

“Ni moja ya mambo ambayo unaisikia na unaanza kuchukua vitu vidogo na unaiona kwenye TV na mahojiano ya wachezaji wengine, kwa hiyo inakuja kawaida zaidi kuliko unavyofikiria.

“Ni rahisi zaidi kuliko kujaribu kujifunza Kijerumani. Nilisoka Kihispania shuleni hadi mwaka wa tisa, ni wazi, kwa kuzingatia nyuma, ningeendelea nayo.

Ahmed Ally: Hatujakurupuka kambi ya Uturuki
Dilunga afunguka kilichomng'oa Simba SC