Baada ya kuanza kazi rasmi huko magharibi mwa jijini London, Kocha kutoka nchini Argentina Mauricio Pochettino anatazamia kupanga mipango ya kuijenga upya Chelsea na kurejesha furaha.

The Blues walimaliza katika nafasi ya 12 kwenye msimamo wa Ligi Kuu England wakiwa na alama 44 msimu uliopita, wakijikusanyia ushindi mara 11 pekee katika mechi 38.

Lakini sasa kuna matumaini makubwa pale Stamford Bridge baada ya kuwasili kwa Pochettino, pamoja na kusajiliwa kwa washambuliaji Christopher Nkunku na Nicolas Jackson.

Pochettino mwenye umri wa miaka 51, alisema: “Tunataka kuleta furaha tena kwa klabu hii kubwa ya soka.

“Historia ya Chelsea ni kushinda, lakini ni muhimu jinsi tunavyoenda kujenga ushindi huo.

“Katika miaka 10, 12, 15 iliyopita, Chelsea, ndiyo timu kubwa zaidi nchini England. Nataka kuifanya iwe ya kusisimua sana kufanya kazi na timu yetu changa na tunaweza kujenga mafanikio katika miaka michache ijayo.”

Pochettino anafurahia fursa hiyo ya kuboresha wachezaji wachanga wenye vipaji wa klabu hiyo.

Aliongeza: “Matarajio ni sisi kwanza kuunda jukwaa kwao kujisikia vizuri sana kwenye uwanja wa mazoezi.  Wanahitaji kuwa na nafasi yao na kujisikia muhimu.

“Utaalamu wetu ni kuipa Chelsea zana bora zaidi kwa wachezaji kuwa na mafanikio, kuboresha kwa njia ya mtu binafsi na ya pamoja, na nadhani tuna uzoefu na kwa pamoja tunaweza kuunda safari nzuri.

“Ikiwa sote tutakuwa pamoja tutakuwa na nguvu kwa sababu tuna kikosi bora na tutaleta wachezaji wenye kujitolea ambao wanataka kuwa sehemu yake.”

Namungo FC kama Young Africans, yaalikwa Burundi
Ahmed Ally: Hatujakurupuka kambi ya Uturuki