Dodoma Jiji imeanza usajili kwa kishindo na sasa imemsajili mshambuliaji wa Kagera Sugar na Taifa Stars, Meshack Abraham.

Mbali na huyo, awali timu hiyo ilisajili wachezaji kadhaa akiwemo beki wa kushoto kutoka Coastal Union, Gustavo Simon.

Kwa upande wa Abraham nyota wa zamani wa Gwambina, amekuwa na msimu bora na timu yake ya Kagera Sugar.

Kiongozi mmoja wa Dodoma Jiji ambaye hakutaka kutajwa jina lake amesema timu hiyo imetoa fedha za maana kupata huduma za wachezaji hao ambao walikuwa wakihitajika na timu nyingi za Ligi Kuu.

“Wa kwanza kusaini alikuwa Gustavo baadaye ndio tukamalizana na Abraham,” amesema kiongozi huyo.

Hata hivyo, kiongozi huyo alisema Dodoma Jiji imeamua kufanya usajili kwa siri na itawatangaza nyota hao hivi karibuni.

Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili wa timu hiyo, Fred Mwakisambwa amesema kuna wachezaji tayari wamewasajili na baadhi wameachana nao watawatangaza hivi karibuni.

“Kuna wachezaji tumeshaachana nao na wengine tumewasajili, tutawatangaza hivi karibuni muda ukifika.”

Maagizo ya Waziri Mkuu kwa makatibu tawala wa wilaya
Habari Kuu kwenye magazeti ya leo Julai 5, 2023