Mshambuliaji Willfred Zaha ameripotiwa kukubali dili mpya kutoka kwenye klabu tatu tofauti.

Winga huyo wa kimataifa wa Ivory Coast, Zaha kwa sasa ni mchezaji huru baada ya mkataba wake huko Crystal Palace kufikia tamati mwishoni mwa mwezi uliopita.

Hata hivyo, Palace bado wanapambana kumshawishi Zaha, 30, asaini dili jipya abaki, wakimpa ofa ya mkataba wa miaka minne wenye thamani ya Pauni 200,00 kwa wiki.

Lakini, kwa mujibu wa Sky Sports, Zaha amekubali dili za klabu nyingine tatu, Lazio, Fenerbahce na Al-Nassr.

Sasa alichobakiza ni kuamua tu ni mkataba wa timu gani asaini kwa ajili ya kuwatumikia msimu ujao.

Uhamisho wa Lazio au Fenerbache utamfanya Zaha akashiriki kwenye michuano ya Ulaya msimu ujao.

Lazio ipo kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya baada ya kumaliza ya pili kwenye Serie A, wakati Fenerbache wamefuzu kucheza Europa League msimu ujao baada ya kumaliza ya pili kwenye ligi ya Uturuki.

Chaguo jingine la Zaha lililopo kwenye meza yake ni kwenda kuungana na Cristiano Ronaldo huko Saudi Arabia. Majina makubwa ya mastaa wa soka wa Ulaya wamekuwa wakihusishwa na timu za Saudi Arabia kwa siku za karibuni.

Tayari mastaa kadhaa wameshakwenda kwenye ligi ya nchi hiyo akiwamo Karim Benzema, N’Golo Kante, Ruben Neves, Kalidou Koulibaly na Edouard Mendy.

Aliyegomea rushwa ya ngono afukuzwa kazi
Geita Gold FC yabisha hodi Zanzibar